Jamii yatakiwa kupiga vita ukatilii kwa watoto
20 June 2024, 13:25
Jamii na wadau wa maendeleo wilayani kasulu mkoani kigoma imetakiwa kushirikiana kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatilii kwa watoto.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Halmashauri ya Mji wa kasulu kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali wameadhimisha sikukuu ya mtoto wa Africa ambayo kimataifa huazimishwa june 16 kila mwaka.
Katika maadhimisho haya mbayo halmashauri ya mji wa kasulu imeadhimisha leo jamii kwa kuujumla imeendelea kuaswa kushirikiana na wadau mbali mbali katika kuhakikisha wanamlinda mtoto na vitendo vya ukatili.
Mgeni rasmi wa maadhimisho haya kaimu mkuu wa wilaya ya kasulu Bw, Hasan Lucas amewaomba viongozi wa Dini kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kuwalinda watoto na ukatili ili watimize ndoto zao.
Awali mtoto Eva Neka akisoma lisala mbele ya mgeni rasimi ametaja mambo kadha wa kadha yanayo wakwamisha kufikia ndoto zao hasa kwa watoto wakike kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Vumilia simbeye amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na halmashauri katika kuhakikisha wanamlinda mtoto na kuendeleza vipaji vyao.
Hata hivyo mratibu wa huduma ya mtoto wilayani Kasulu kutoka shirika la compassion Bw,Stevin Kalbwami amesema ni wakati wa kukemea kwa nguvu zote unyanyasaji kwa watoto unaowapelekea wasifikia malengo yao.