Joy FM

Jamii yatakiwa kuwathamini watoto Kasulu

19 June 2024, 12:18

Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara, Picha na Mwanahabari wetu

Kutokana na vitendo vya ukatilii vinavyoendelea kushamili kwa watoto kwenye wadau wametakiwa kuunga mkonojuhudi za kuwalinda watoto.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Jamii wilayani kasulu Mkoani Kigoma imetakiwa kuwathamini watoto kwa kuwapatia mahitaji yao ya msingi ikiwemo huduma za afya mavazi malazi na lishe bora.

Kikao cha shirika la world vision Tanzania kiliwakutanisha waalimu wakuu wa shule za msingi, na sekondari,wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari,viongozi wa dini, wazazi na walezi katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanywa na shirika hilo katika kata ya makere.

Kaimu mkurugenzi wa mradi wa Buhoma kutoka shirika la World vison Tanzania bw.Emmanuel Ntachombonye amesema baadhi ya watoto hawapati mahitaji yao ya msingi kutokana na baadhi ya wazazi kuwatelekeza na kwenda kufanya shughuli za kilimo shambani.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi wa mradi wa Buhoma kutoka shirika la World vison Tanzania bw.Emmanuel Ntachombonye

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya kasulu bw.Jalali kiumbe amesema migogoro ya ndoa imechangia baadhi ya watoto kushindwa kupata mahitaji yao ikiwemo afya,elimu,na mavazi.

Sauti ya Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya kasulu Bw. Jalali kiumbe

Akizungumza kwa niaba ya katibu Tawala wilaya ya kasulu afisa Tarafa ya makere bw.Paul Ramadhani ameiomba jamii kuacha ubaguzi na unyanyasaji kwa watoto ili kuwainua katika elimu ambayo itawasaidia kufikia malengo yao.

Sauti ya katibu Tawala wilaya ya kasulu afisa Tarafa ya makere bw.Paul Ramadhani