Waislamu wametakiwa kuwajali wasiojiweza
17 June 2024, 15:34
Wakati waislamu duniani kote wakiwa wameungana kusherekea siku ya Eid El Hajj wito umetolewa kwao kuendelea kuwasaidia watu wasiojiweza hasa wanaishikatika mazingira magumu.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameaswa kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa amani, uturivu na kuwajali wasiokuwa na uwezo kwa kuwapatia sadaka
Waislamu kote nchi wameungana kuadhimisha sikukuu ya Eid ambapo sala zimefanyika katika maeneo mbalimbali radio joy fm imefika katika msikiti wa ijumaa wa BAKWATA Kasulu mji na kuzungumza na shekhe mkuu wa wilaya hiyo Shekhe Masoud Swedi Kikoba ambaye amewasisitiza waumini hao kusherehekea kwa amani na pasipokutenda matendo maovu.
Aidha Shekhe Kikoba ametoa wito kwa viongozi wa serikali kufanya kazi zao kwa uadilifu ili kuleta maendeleo katika taifa hili la Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye amewaomba wanananchi kuendelea kuiombea serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wake katika shughuli za kuwaletea maendeleo.
Nao baadhi waumini wa dini ya kiislamu Wilayani Kasulu wamesema ni jukumu lao kuilinda amani na kuendelea kusaidiana wao kwa wao.