Usafirishaji holela wa kemikali ziwa Tanganyika hatari kwa viumbe
14 June 2024, 09:13
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya usafirishaji wa kemikali kupitia ziwa Tanganyika ili kusaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza iwapo wasafirishaji hawatazingatia usafirishaji bora wa kemikali.
Na Kadilsaus Ezekiel – Kigoma
Wasafirishaji wa Bidhaa mbalimbali katika nchi jirani za Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kupitia ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, wameomba Serikali kudhitibi usafirishaji holela wa kemikali kunusuru milipuko ambayo inaweza kusababisha madhara na hasara ikiwemo kuhatarisha uhai wa binadamu.
Baadhi ya wadau wa usafirishaji mkoani kigoma, wamesema ukosefu wa elimu ya utambuzi wa kemikali huenda ikasababisha milipuko wakiwa kazini, kutokana na uwepo wa madini yanayosafirishwa kutoka nchi jirani, na kuingizwa mkoani Kigoma.
“wengi wetu hatuna elimu ya masualaya kemikali kwahiyo unakuta tunasafirisha kwa kutumia uzoefu tu na pia inategemea na aina gani ya madini unayotakakusafirisha na hasa carboni ndio tumekuwa tukisafirisha”
Kwa upande wake meneja wa Bandari za ziwa tanganyika davis mabula amesema kemikali nyingi zinazosafirishwa zinatokea nchi jirani ya Congo na wamekuwa wakidhiti kwa kufanya ukaguzi, huku mkurugenzi wa huduma za udhibiti mamlaka ya kemikali serikalini daniel dio akihakikisha usalama kwa kuendelea kuelimisha jamii.
Aidha mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kigoma mheshimiwa Thobias Andengenye, afisa biashara mkoa wa kigoma Deograius Sangu, amesema kutokana na kemikali hizo kuathili jamii ni wajibu sheria zifuatwe kulinda rasrimali watu.