Joy FM

“LATRA chukueni hatua kwa wanaokiuka sheria”

13 June 2024, 09:32

Mkuu wa wilaya kigoma Mh. Salum Kalli akiwa na kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wengine wakiwa stendi kuu ya mabasi kigoma masanga, Picha na Josephine Kiravu

Mkuu wa Wilaya Kigoma Mh. Salum Kalli amewataka wasimamizi wa wa vyombo vya usafiri kuhakikisha madereva na wamili wa mabasi yaendayo mikoani wanazingatia kanuni za usalama barabarani ili kuzuia ajali za barabarni.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Abiria wanaosafiri kutokea mkoani Kigoma kuelekea mikoa mbalimbali hapa nchini wamezitaka mamlaka zinazosimamia usafiri wa ardhini kuondoa changamoto ya abiria kukatiwa tiketi inayoonesha siti moja kwa zaidi ya mtu mmoja.

Hayo yamejiri wakati mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli alipotembelea eneo la stand kuu ya mabasi mkoani kigoma nakuzungumza na abiria,madereva pamoja na mawakala wa kukata tiketi katika eneo hilo.

Mkuu wa wilaya kigoma Salum Kalli akizungumza na Mkuu wa usalama barabarani wilaya ya kigoma wakati wakiwa katika stendi kuu ya mabasi kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Akiwa katika eneo hilo la Masanga mkuu wa wilaya ametoa maelekezo kwa LATRA kufanya kazi kwa weledi hasa katika kipindi ambapo baadhi ya mabasi hufanya safari zake nyakati za usiku kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Dar es salaam na Mwanza.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kalli

Na hapa Mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Kigoma ibrahimu Mbarouk wamesisitiza madereva kufuata sheria pamoja na wamiliki wa mabasi kuhakikisha madereva wanakuwa wawili ili kudhibiti ajali za barabarani.

Sauti ya mkuu wa usalama barabarani wilaya ya kigoma

Katibu wa KIBOTA Nuhu Salum nae akatia neno kwa kuiomba Serikali kuimarisha ulinzi ndani ya stendi hiyo pamoja na kuona haja ya kuweka mazingira rafiki kwa abiria wanaotoka vijijini ambao wanalala ndani ya stendi hiyo.

Katibu wa KIBOTA Nuhu Salum nae akatia neno kwa kuiomba Serikali kuimarisha ulinzi ndani ya stendi, Picha na Josephine Kiravu

Nao baadhi ya mawakala wa kukata tiketi katika stendi hiyo ya mabasi wamesema ili kuondoa changamoto ya abiria kukatiwa tiketi yenye siti moja kwa zaidi ya mtu mmoja wanapswa kufika kwenye ofisi halali za mabasi na sio kwa wapiga debe.