Joy FM

5 wafariki, 5 wajeruhiwa ajalini uvinza

12 June 2024, 09:21

Picha ya gari lililopata ajali na kuacha majeruhi, Picha na Mtandao

Majeruhi wa ajali iliyotokea siku ya Jumapili wakati wafanyakazi wa kampuni ya Tropical Estate Grid Electricity Ltd, inayosambaza umeme wa REA vijijini Pamoja na vibarua wakitoka katika shughuli zao katika Kijiji cha Rubalesi wakielekea Kijiji cha Rukoma wameanza kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Na Emmanuel Matinde – Uvinza

Majeruhi watatu kati ya watano waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni mkoa wa Kigoma kufuatia ajali iliyohusisha gari aina ya fuso katika Barabara ya Ikuburu-Katare katika kijiji cha Rukoma wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wameruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Maweni Dkt. Habakuki Ntabudyo, amesema jana Jumatatu walipokea majeruhi watano waliotokana na ajali hiyo wakiwa wameumia sehemu mbali mbali za miili yao na kuanza kuwapatia huduma.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Maweni Dkt. Habakuki Ntabudyo

Ajali hiyo imetokea siku ya Jumapili wakati wafanyakazi wa kampuni ya Tropical Estate Grid Electricity Ltd, inayosambaza umeme wa REA vijijini Pamoja na vibarua wakitoka katika shughuli zao katika Kijiji cha Rubalesi wakielekea Kijiji cha Rukoma, ambapo Meneja Mradi wa Kampuni hiyo ni mmoja wa majeruhi ameelezea ajali hiyo ilivyotokea.

Sauti ya Meneja Mradi wa Kampuni ya Tropical Grid Electricity Ltd

Awali akitoa taarifa ya ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Filemon Makungu, amesema chanzo cha ajali ni gari kuacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi wanane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Filemon Makungu
Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Filemon Makungu