“Wakulima tumieni mbegu bora za kahawa”
10 June 2024, 10:48
Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma inatarajia kugawa mbegu bora za kahawa kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija ambacho kitakuwa na mazao ya kutosha na yenye ushindani kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Na Michael Mpunije
Wakulima wa zao la kahawa wilayani Kasulu mkoani kigoma wametakiwa kufuata hatua bora za kilimo hicho kwa kutumia miche bora yenye uwezo wakukabiliana na magonjwa yanayo shambulia zao hilo ili kuleta ufanisi kupitia kilimo hicho.
Hayo yamejiri katika kikao kuwajengea uwezo wa kulima wa zao la kahawa na maafisa ugani kutoka halmashauri ya mji kasulu na halmshauri ya wilaya ya Kasulu ambapo kilimo hicho kinatajwa kuleta tija kwa wakulima wazao hilo ikiwa watazingatia hatua bora za kilimo.
Akizungumza mara baada ya kutamatika kwa mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku mbili kiongozi kutoka kituo kidogo cha utafiti wa kahawa Tacri mwayaya bi Sophia malinga amewataka wakulima kuacha kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikichelewesha mafanikio yao.
Baadhi ya wakulima viongozi ambao wameshiriki katika mafunzo hayo Yosamu zefania na Aneth ntamsano wamesema watahakikisha wanatoa Elimu kwa wakulima wengine ili kuleta matokeo chanya ambayo yatasaidia kukuza uchumi wao huku wakiomba kuwepo soko la uhakika la zao hilo.
Mratibu wa kahawa katika halmashauri ya mji kasulu bw Eliakimu john amesema wamezalisha zaidi ya miche milioni 1 ambayo wanatarajia kuigawa kwa wananchi mapema mwezio oktoba wakati wa maandalizi ya kilimo.