Joy FM

“Kasulu ni shwari licha ya uwepo viashiria vya uvunjifu wa amani”

7 June 2024, 12:02

Mkuu wa wilaya kasulu kanali Isac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali wilayani Kasulu imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo udokozi na wizi kwenye makazi yao ili kuhakikisha wananchi kufanya kazi kwa amani.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu amesema hali ya usalama katika wilaya hiyo iko vizuri kuhakikisha mwananchi anafanya shughuli zake za kimaendeleo kwa amani.

Kanali Mwakisu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema licha ya usalama uliopo lakini zipo baadhi ya changamoto ndogo ndogo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu

Aidha Kanali Mwakisu amezungumzia namna ambavyo serikali imeendelea kuweka mikakati bora ya kutatua changamoto hizo maana usalama unapokuwepo unamsaidia mwananchi kufanya shughuli za kimaendeleo na kuweza kujiingizia kipato kitakachomsaidia yeye na jamii yake yote inayomzunguka.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu

Katika hatua nyingine Kanali Mwakisu ameipongeza serikali kwa kuendelea kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi kwa kulituma jopo la Mawaziri nane waliofika mkoani hapa ili kuhakikisha sehemu ambazo zina migogoro ya ardhi zinatatuliwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu