Wakimbizi waishio kambi za Kigoma watakiwa kurudi kwa hiari
7 June 2024, 11:48
Serikali ya Tanzania na Burundi zimeendelea kuhamasisha wakimbizi waishio kambi za nduta na nyarugusu mkoani kigoma kurejea kwao kwa hiari kwani tayari taifa la burundi kuna amani ya kutosha kwa sasa.
Na, Josephine Kiravu
Kufuatia kusuasua kurejea makwao wakimbizi wa Burundi waliopo kambi za wakimbizi Mkoani Kigoma, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Burundi wameamua kwa pamoja kufanya zoezi muhimu kwa ajili ya kuwarejesha kabla ya mwezi 31 Disemba mwaka huu kwani hali ya usalama nchini Burundi kwani sasa ipo shwari.
Waziri wa Mambo ya ndani hapa nchini Tanzania mhandisi Hamad masaun amesema nia ya Serikali kuhusu kurejea nchini mwao wakimbizi kutoka Burundi ambao hadi sasa wapo kwenye kambi za wakimbizi.
Amesema tangu mwaka 2017 mchakato wa kuwarejesha wakimbizi raia wa Burundi ulianza lakini hata hivyo licha ya vikao kadhaa kuketi bado wengi wao wamekuwa hawataki kurejea nchini mwao licha ya hali ya usalama kwa sasa kuwa shwari.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani maendeleo ya jamii na usalama wa raia nchini Burundi Theophile Ndarufatiye amesema kuna haja serikali ya Tanzania kuweka mkazo kwa wakimbizi hao kurejea nchini mwao kwani hadi sasa wapo takribani laki moja hapa nchini Tanzania na matarajio yao ni kuona angalau kwa wiki moja wanarejesha wakimbizi 2000.
Naye mkuu wa mkoa wa kigoma amesisitiza kurejea kwa hali ya usalama nchini Burundi na kuwataka wakimbizi wote kurejea nchini mwao ili kulijenga taifa lao.
Waziri Masauni amehitimisha kikao cha siku mbili cha wataalamu wanaoziwakilisha nchi za Tanzania na Burundi ambacho kimelenga kujadili urejeaji wa wakimbizi waliopo nchini kutokana na hali ya amani na utulivu kutengemaa nchini humo.