Bidhaa zateketea kwa moto, maduka 12 yakinusurika Kasulu
5 June 2024, 13:15
Wananch wilayani kasulu mkoani kigoma kuendelea kuchukua tahadhari za majanga ya moto ili kuepuka hasa zinazojitokeza baada ya kutokea majanga ya moto.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Duka moja limeungua kwa moto katika soko kuu la Kasulu Mjini lililopo jirani na eneo la round about kata ya Kumsenga halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma likiwa na bidhaa ya mabegi huku zaidi ya maduka 12 yakinusurika kuungua kwa Moto.
Ni Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Boaz Saigoni, Dunia Ndebheimana, Elibariki Alex na Enos Kaele wameeleza kile walichokiona kuwa ni chanzo cha duka hilo kuwaka moto.
Kwa upande wake Mmiliki wa duka hilo ambalo limewaka moto Bw, Danfrod John amelishukuru Jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na baadhi ya wananchi kwa kuokoa baadhi ya bidhaa zilizokuwa ndani ya duka hilo sambamba na kubainisha thamani ya vitu vilivyoungua.
Naye Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Kasulu Inspector Anthony Marwa amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wafanyabiashara kuwa na vifaa kinga vya moto pamoja na kutoa taarifa za haraka pindi majanga ya moto yanapotokea.