Uchafuzi wa mazingira watajwa kuathiri ziwa Tanganyika
4 June 2024, 13:32
Shughuli za binadamu zimeendelea kutajwa kama chanzo kikuu cha uchafuzi wa mazingira katika ziwa Tanganyika na kusababisha viumbe vilivyomo ndani ya ziwa hilo kuwa hatarini.
Na Tryphone Odace
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika wamekutana na kujadili njia bora kulinda na kuhifadhi ziwa Tanganyika ili kulinusuru na uhalifu unaotokana na shughuli za binadamu ikiwemo utiririshaji maji taka.
Ziwa Tanganyika hutegemewa na takribani watu milioni 12 kutoka nchi hizo kwa ajli ya kuendesha maisha yao kupitia shughuli za uvuvi lakini kama chanzo kikubwa cha maji kwa jamii hiyo.
Uhai na uendelevu wa ziwa Tanganyika na viumbe wengine kama samaki hutegemea utunzaji na hatua madhubuti ya kudhibiti utupaji wa taka ngumu utiririshaji wa maji taka na shughuli zote za binadamu kama anavyoeleza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto Thobias Andengenye mara baada ya kufungua kikao cha kujadili mikakati ya kulinda ziwa hilo dhidi ya uharibifu unafanywa na jamii za nchi hizo zinazilizunguka ziwa Tanganyika.
Magayane Silas ni mdau wa mazingira kutoka wilaya ya Nyanzalac mkoani Makamba nchini Burundi amesema kuwa shughuli za binadamu ni miongoni mwa vitu vinavyoathiri ziwa, uendelevu wa Tanganyika na viumbe vilivyomo.
Kwa upande wake mratibu wa shirika la UN Habitat Tanzania Bw. Stansalua Nyembea amesema kikao hicho kitajikita kutafuta njia sahihi ya kukabiliana na changamoto zinazolikabili ziwa Tanganyika.