Joy FM

Mwalimu mbaroni kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wake

30 May 2024, 10:06

Ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mkugwa iliyopo Kibondo, Picha na Kadislaus Ezekiel

Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria walimu na watu wote ambao wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi wao kwani wanasababisha kwanafunzi kushindwa kufikia malengo yao.

Na Kadislaus Ezekiel – Kibondo

Jeshi  la Polisi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, limemkamata Mwalimu wa shule ya Sekondari Mkugwa Girls High School, jina limehifadhiwa, kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanafunzi wa Shule hiyo akiwa nyumbani kwake na kusababisha baadhi yao kukatiza masomo.

Wakizungumza na kituo hiki, baadhi ya walimu na wanafunzi, wamekili mwalimu huyo amekutwa akiwa amelala na mwanafunzi wake wa kidato cha tano baada ya kufanya uchunguzi wa kina wakiwa na baadhi ya Polisi nyakati za Usiku.

Sauti ya walimu na wanafunzi wakizungumzia tukio la mwalimu kukutwa amelala na mwanafunzi wake

Mkuu wa shule ya Mkugwa Girls High School Mwalimu Mather Kajoro amesema kamati ya shule imeshakaa na mwalimu huyo na kumchukulia hatua za kinidhamu bila mafanikio, wakati Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo Rutema Mugishagwe amesema mtuhumiwa kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi kwa hatua za kisheria zaidi.

Sauti ya Mwalimu mkuu wa Mkugwa na mkurugenzi wilayani kibondo

Kibao cha shule ya sekondari ya wasichana ya Mkugwa Kibondo