Wananchi acheni kusema maji ni ya Mungu, lipieni ankara za maji.
30 May 2024, 09:30
Mamlaka zinazosimamia huduma za maji zimetakiwa kuhakikisha zinasambaza huduma ya maji maeneo yote ambayo hawajafikia huduma ya maji.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye umetoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya kigoma kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu na mamlaka zinasimamia huduma ya maji illi kusambaza mtandao wa maji kwenye maeneo na vijiji ambayo havijafikiwa na huduma ya maji safi na salama
Andenge ametoa kauli kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya kigoma.
Amesema dhamila ya Serikali ya awamu ya sita nikuona wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao, huku akitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kusema maji ni ya Mungu badala yake wachangie kulipia Ankara za maji.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri hiyo Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini KUWASA mhandisi Alone Kaje amesema licha ya jitihada za serikali kuwasambazia wananchi huduma ya maji wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo baadhi ya wananchi kukataa mambo ya maji yasipite kwenye maeneo yao na mvua zilizonyesha zimeharibu baadhi ya vyanzo vya maji.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi na viongozi wa jumuiya za watumia maji wa Halmashauri hiyo wamesema watotoa ushirikia kwa viongozi wa wanaosimamia maji ili kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi.
Mpango wa serikali nikuhakikisha ifikapo mwaka 2025 huduma ya maji safi na salama iwe imefika vijijini kwa asilimia 85 na mijini kwa asilimia 95.