Joy FM

Wananchi watakiwa kutunza mazingira Kigoma

28 May 2024, 13:07

Baadhi ya magogo ya miti yalliyokatwa ikiwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira, Picha na Tryphone Odace

Wananchi  mkoani  Kigoma wametakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kurejesha ardhi kwenye uoto wake wa asili, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Na Timotheo Leonard – Kigoma.

Zaidi ya hekta laki nne za misitu hupotea kila mwaka nchini tanzania kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uanzishwaji wa mashamba mapya ya kilimo, ukataji miti kiholela kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa na upasuaji mbao.

Kauli hiyo imetolewa na  Meneja wa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira Kanda ya magharibi NEMC, kanda ya magharibi kuelekea wiki ya mazingira duniani  wakati akiongea   na redio joy fm na kueleza kuwa utunzaji wa mazingira ni wajibu kila mwananchi.

Meneja wa NEMC kanda ya magharibi akizungumzia siku ya mazingira duniani, Picha na Tryphone Odace

“Tumetoa elimu ya kutosha juu ya utunzanji wa mazingira hasa kuwahamasisha wananchi kuzingatia usafi wa mazingira na kutokata miti”

Sauti ya meneja wa NEMC Kanda ya Magharibi

Hata hivyo Bw, Mgila amesema katika kufikia mpango wa serikali wa kuwa na 80% ya watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia kufikia mwaka 2034 ,maeneo yote nchini yenye vituo vya mafuta kutakuwa na vituo maalum vya gesi ili wananchi waipate kwa urahisi.

Sauti ya meneja wa NEMC Kanda ya Magharibi

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanatarajia kuanza Juni mosi Mwaka na kufikia kilele Juni 5 mwaka huu yakienda sambasamba na kaulimbiu ya urejeshwaji wa ardhi, ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame.