Joy FM

Wazee waomba serikali kuongeza pesa za TASAF

28 May 2024, 11:16

Wanufaika wa TASAF buhigwe, Picha na Kadislaus Ezekiel

Licha ya serikali kuendelea kutoa pesa kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini kwa kaya ambazo hazijiwezi, baadhi ya wanufaika wameomba serikali kuendelea kuongeza kiasi cha fedha ambazo zitasaidia walengwa kujikwamua zaidi.

Na Kadislaus Ezekiel – Buhigwe

Wazee katika halmashauri ya wilaya ya buhigwe mkoani kigoma, ambao ni wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini tasaf, wameiomba serikali kuona namna ya kuongeza kiasi cha fedha wanachopatiwa ili kunufaika zaidi kwa kufanya maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza na viongozi wakati wa mkutano wa kutatua kero na changamoto zinazowakabili wazee, wamesema licha ya kuanzisha miradi ya ufugaji wa mbuzi na kuku, ambayo imewasaidia baadhi yao kujenga hata nyumba za makazi, bado wanadai kiwango cha fedha wanachopatiwa ni kidogo ikilinganishwa na hali zao kiuchumi, na kuomba serikali kuendelea kuwajali.

Sauti ya wazee ambao ni wanufaika wa mpango wa tasaf Buhigwe

Kwa upande wake, Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini tasaf halmashauri ya wilaya ya buhigwe rojadeter mwanri, ameeleza mikakati ya kuongeza fedha kwa wazee kuwa, wanatakiwa kuongeza wategemezi wanaowasaidia kufanya kazi na kwamba hadi sasa zaidi ya bilioni tano zimetolewa na serikali kwa kipindi cha miaka mitatu kusaidia ustawi wa wazee.

Sauti ya mratibu wa tasaf Buhigwe