Joy FM

Serikali kuboresha miundombinu kwa wanafunzi walemavu

23 May 2024, 09:05

Ni mwanafunzi wa shule ya msingi kasulu mwenye ulemavu akiwa kwenye kiti mwendo, Picha na Hagai Ruyagila

Wadau wa maendeleo wametakiwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanatengeneza miundombinu wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili weweze kusomea katika mazingira rafiki.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wito umetolewa kwa serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya shule kwa watoto wenye mahitaji maalum katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma ili waweze kusomea kwenye mazingira rafiki sawa na watoto wengine.

Wito huo umetolewa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kasulu Rose Kibindi wakati akizungumza na Radio Joy fm nakusema kuwa licha ya jitihada za seriakali katika kuboresha miundombinu ya shule kwa watoto wenye mahitaji maalum shule anayoiongoza bado baadhi ya miundombinu hairidhishi.

Sauti ya mkuu wa shule ya msingi kasulu Bi Rose Kibindi

Kwa upande wake Afisa elimu kata ya Murusi Gervas Lugeze ambaye amemuwakilisha afisa elimu, elimu ya watu wazima halmashauri ya Mji Kasulu amekiri uwepo wa changamoto ya miundombinu kwa baadhi ya vituo vinavyotoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, lakini amesema serikali imepokea na itazifanyia kazi ili kutatua changamoto hizo.

Sauti ya afisa elimu kata ya mrusi kasulu

Katika hatua nyingine Lugeze amesema muamko wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata elimu ni mkubwa ndivyo serikali itaendeleoa kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum shule.

Sauti ya afisa elimu kasulu

Kata ya Murusi ina vituo viwili vinavyotoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ambapo cha kituo cha kwanza kinapatikana katika shule ya msingi Kasulu na kingine katika shule ya msingi Bajana.