Joy FM

Silverlands yawapa elimu ya ufugaji kuku zaidi ya wafugaji 200

22 May 2024, 08:12

Baadhi ya wafugaji wa kuku mkoani Kigoma wakipatiwa mafunzo ya ufugaji bora na kampuni ya silverlndas, Picha na Mwandishi wetu

Wafugaji wa kuku mkoani Kigoma wamesema kuwa wana nia na dhamira ya kufanya ufugaji wa tija kwa kuwa uvuvi kuwa ni miongoni mwa biashara ambayo inaweza kuinua kila mtu na kukuza uchumi wake na taifa kwa ujumla.

Na Tryphone Odace – Kigoma

Zaidi ya wafugaji wa kuku 200 mkoani Kigoma wamepatiwa mafunzo ya namna ya ufugaji bora wa kuku na wenye tija kwa ajili ya biashara kutoka kampuni ya Silvalandas yanye makao makuu mkoani Iringa ambapo wameeleza kuwa kupitia elimu hiyo huenda wakaepukana na ufugaji ambao hauna tija kama ilivyokuwa imezoeleka.

Meneja Mauzo kutoka kampuni ya Silvelrands inayojihusisha uzalishaji wa vifaranga na chakula cha kuku Bw. Jaremiah Kilato alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha ufugaji wa kisasa na wenye tija na kuwa mkoa wa Kigoma umepewa kipaumbele kutokana na mwamko mkubwa wa wafugaji wa mkoa huo kuamua kufanya uwekezaji mkubwa kupitia ufugaji wa kuku kama ilivyo biashara nyingine.

“Kama kampuni tumepita mikoa yote ya Tanzania na kuona mkoa huu watu wanahitaji kupatiwa elimu ya ufagaji wa kuku lakini pia hata kufahamu njia bora za ufagaji na namna ya kuanda vyakula kwa kuku wanaofugwa na hivyo tumekuja kuhakikisha tunawapa elimu lakini pia wafahamu tutakuwa karibu nao ili waweze kuona matunda ya ufagaji wa kuku”.

Mtalaam akiwa anatoa elimu ya ufugaji wa kuku, Picha na mwandishi wetu

Bw. Kilato alisema Kutokana na mwamko huo uhitaji wa bidhaa za kampuni hiyo umekuwa mkubwa hivyo kampuni imeamua kuweka uwakilishi wa moja kwa moja ambapo kuna mawakala ambao wanasaidia kuuza bidhaa hizo ili kuunga mkono juhudi za wafugaji ambao walikuwa wakitumia muda mrefu kusafiri kwenda kutafuta vyakula vya kuku lakini aina gani ya kuku wanaweza kuhimili hali ya hewa sehemu walipo.

Nao baadhi ya Wafugaji wa Kuku mkoani Kigoma akiwemo Temba Gudila wailisema kuwa ufugaji wa kuku wenye tija ni miongoni mwa biashara ambayo inaweza kuwasaidia kuinua kila mtu atakayekuwa tayari kufanya ufugaji kwa kufuata utalaamu.

Hayo yalielezwa Gudila Temba mfugaji wa kuku kutoka Mkoa wa Kigoma wakati wa mafunzo ya kilimo na ufugaji yaliyotolewa na kampuni ya silverlands yenye makao yake makuu mkoa wa Iringa yaliyofanyika kwa wafugaji wa mkoa wa Kigoma.

“Natarajia kufanya ufugaji wa tija zaidi, nimegundua ufugaji ni biashara mimi binafsi nilianza na kuku 100 tena kwa kuwanunua kwa mfugaji mwenzangu lakini kupitia hao kuku nimefikia kuku zaidi ya 2000 na sasa naendelea kukua” alisema Temba.

Hata hivyo Silverlands imeona ni vyema kutoa mafunzo kwa wafugaji ikiwa ni sehemu ya kazi zao na ni mafunzo ambayo mfugaji wa kuku anatakiwa ayapate ili kuboresha ufugaji wa kuku aina ya kuku nyama, kuku mayai na chotara.

Afisa uhusiano wa kampuni ya Silverlands akitoa elimu kwa wafugaji wa kuku, mafunzo ambayo yamefanyika ukumbi wa social hall, Picha na mwandishi wetu

Mafunzo hayo ni pamoja na sehemu ya usimamizi wa miradi, ulishaji kuku, utoaji chanjo na utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kupata uelewa wa kuwakinga kuku na magonjwa ambayo imekua changamoto inayosababisha wafugaji kukata tamaa na wakati mwingine kuua mitaji yao.

Akizungimzia masuala la ya chanjo Bi. Happy Tendega kutoka kampuni ya CEVA amesema kuwa, kuku anapaswa kuchanjwa akiwa kifaranga ili kuepuka magonjwa yote wanayomkabiri, ambapo miangoni wa chanjo ni kideri na mafua.

Aidha alisema kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kienyeji bila kufuata utaalamu na hivyo kutoona manufaa ya ufagaji wa kuku na kuwataka wafugaji kuendelea kuzingatia kanuni Bora za ufagaji.

Elimu ya ufugaji wa kuku ikiendelea kutoa na watalaamu kutoka kampuni ya Silverlands, Picha na Mwandishi wetu