Joy FM

Kasulu: Zingatieni vipimo vya dawa ya kutibu maji

21 May 2024, 11:47

Wananchi wakiwa wanateka maji katika moja ya kituo cha maji wilayani Kasulu, Picha na michael Mpunije

Dawa inayotumika kutibu maji kwenye vyanzo vya maji kabla ya kumfikia mtumiaji huenda vipimo vikawa havizingatiwi kutokana na wananchi kulalamikia maji yanatoka kuwa na hali ya dawa na kuwaacha na hofu kuwa wanaweza kupata madhara.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wadau wa huduma ya maji kwa wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia vipimo sahihi vya dawa ya kutibu maji inayowekwa kwenye visima ili kuondoa harufu mbaya kwenye maji ambayo imekuwa ikileta changamoto kwa watumiaji.

Akizungumza kwenye kikao cha shirika la Water Mission, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw. Semistatus Mashimba amesema harufu mbaya ya dawa inayowekwa kwenye maji imekuwa ikileta sintofahamu kwa watumiaji wa maji hayo kutokana na kukosa elimu.

Amesema wananchi wengi wao huingiwa na hofu wakati wa kutumia maji hayo kutokana harufu ya dawa hizo.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Kasulu

Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Kasulu bi.Theresia mtewele amesema ni vyema wataalamu kuangalia namna ya kuzingatia vipimo sahihi vya kuweka dawa kwenye maji kulingana na kiwango cha maji yaliyopo kwenye kisima.

Sauti ya Katibu Tawala wilaya Kasulu

Naye injinia wa maji kutoka shirika la watermission wilayani Kasulu mhandisi Christopher malenge amekiri kuwepo kwa changamoto  hiyo na kwamba tayari wanaendelea kutoa elimu kwa wataalamu wanaosimamia zoezi la kutibu maji kwenye visima ili waweze kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo hivyo.

Sauti ya injia wa maji kutoka shirika la Water Mission