Joy FM

Afariki kwa shoti ya umeme akiiba nyaya

17 May 2024, 16:18

Nguzo ya umeme, Picha na Michael Mpunije

Wizi na uharibifu wa miundombinu ya umeme umeendelea kushamiri nchini na kusababisha vifo kwa wanaohujumu miundombinu hiyo.

Na Michael Mpunije

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 17 hadi 20 mkazi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kuiba nyaya za umeme kwenye transfoma ya umeme Kiganamo halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma.

Sauti ya mashuhuda wa tukio

Mamashuhuda hao wanasema hilo ni fundisha wenye tabia kama hiyo na haya ndio madhara ya wizi hawakuishia hapo wakathibitisha na usemi kwamba heri kidogo cha halali kuliko kikubwa cha Haramu

Sauti ya wananchi wa mji Kasulu

Meneja wa TANESCO wilaya ya Kasulu mhandisi Danford Yungu  amethibitisha kuwepo kwa tabia ya wizi wa nyanya za umeme na kwamba kulingana na tukio hilo limewasikitisha kwakuwa zipo njia mbalimbali za halali ambazo vijana wakizitumia itawasaidia kujiingizia kipato.

Sauti ya Meneja wa Tanesco wilaya Kkasulu

Waswahili walisema siku za mwizi ni arobaini na hapa Mhandisi Danford anaendelea kusisitiza jamii kuacha tabia ya wizi sanjari na kuepuka kufanya shughuli mbalimbali kwenye maeneo hatarishi hasa katika njia zinazopitisha nyaya za umeme.

Sauti ya meneja wa tanesco wilaya ya Kasulu