Joy FM

Wavuvi Kigoma wapewa maboya kujikoa wakiwa ziwani

17 May 2024, 13:00

Mkuu wa wilaya Kigoma akikabidhi maboya kwa wavuvi ndani ya Ziwa Tanganyika, Picha Hamis Ntelekwa

Serikali imewataka wavuvi wanaofanya shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika kuchukua tahadhari wakiwa ziwani ili kujinga na majanga ya kuzama majini wakiwa wanaendelea na shughuli za uvuvi.

Na Orida Sayon – Kigoma Mc

Jumla ya vifaa vya uokoaji maboya 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.1 yamegawiwa kwa wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kali katika ugawaji wa maboya  kwa wavuvi katika manispaa ya Kigoma Ujiji uliofanyika katika mwalo wa Katonga ambapo amewataka jeshi la zima moto na uokoaji kuendelea kutoa elimu namna ambavyo maboya hayo wanavyotumika.

Sauti ya DC Kigoma Mh. Salum Kalii

Kwa upande wake Kaimu Kamanda Jeshi la zima moto na uokoaji inspekta Jacob Chacha amesema wataendelea kutoa elimu kwa wavuvi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka ziwa Tanganyika ili waweze kujiokoa pindi majanga yanapotokea wawapo katika shuguli zao.

Sauti ya kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto

Nao baadhi ya wavuvi waliopata vifaa hivyo vya uokoaji  wameishukuru serikali kwa kuwapatia vifaa pamoja na kupewa elimu kwa namna ambavyo hutumika katika kutoa msaada wakati wanapokutana na majianga majini.

Sauti ya wavuvi wanafanya shughuli ndani ya Ziwa Tanganyika

Watu waliopewa vifaa hivyo ni pamoja na kikundi cha BMU Kibirizi, BMU Katonga, Ushirika wa wavuvi Kibirizi na Ushirika wa wavuvi Katonga.

Mkuu wa Wilaya Kigoma akimvalisha boya mvuvi anayefanyakazi ziwa tanganyika, Picha na Hamis Ntelekwa