Joy FM

Watumishi wa serikali watakiwa kusimamia ukusanyaji mapato

15 May 2024, 12:59

Muonekano wa majengo ya halmashauri ya wilaya kasulu mkoani kigoma, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali wilayani kasulu mkoani kigoma imesema itandelea kushirikiana na viongozi wote ngazi za chini katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ili yaweze kusaidia katika utelekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Na Hagai Ruyagila – Michael Mpunije

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amepongeza jitihada zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika kwa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kuhamia katika jengo lake jipya la ghorofa moja lililopo katika kijiji cha Nyamnyusi.

Kanali Mwakisu ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la halamshauri hiyo ambapo ameelekeza kuongeza kasi katika kukamilisha maeneo ambayo bado hayajakamilika.

Sauti ya mkuu wa wilaya kasulu kanali Isack Mwakisu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Eliya Kagoma amesema ni jambo la kujipongeza kwa hatua waliyofikia kwani haikuwa kazi rahisi.

Majengo ya halmashauri ya wilaya kasulu mkoani kigoma, Picha na Hagai Ruyagila

Aidha Kagoma amesema ukamilishaji wa baadhi ya ofisi ambazo hazijakamilika unaendelea na kwamba rai yake ofisi hizo kukamilishwa haraka iwezekenavyo ili zihamie eneo hilo kuhudumia wananchi.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashari ya wilaya kasulu

Hivi karibuni katika ziara zake wilayani Kasulu Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna mstaafu wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alitoa maagizo na kuta jengo hilo kukamilishwa ili lianze kutoa huduma kwa wananchi.