Joy FM

Viongozi watakiwa kutoa taarifa za miradi kwa wanahabari

15 May 2024, 12:30

Mkuu wa mkoa kigoma akiwa na wanahabari na viongozi wengine katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, Picha na Tryphone Odace

Viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani kigoma wametakiwa kuwa karibu na wanahabari ili kufahamu miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

Na Lucas Hoha – Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewataka viongozi wa serikali kwenye halmashauri za mkoa wa Kigoma kutoa taarifa na ushirikiano kwa waandishi wa habari ili wananchi wapate taarifa sahihi zinazohusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Mh. Andengenye ametoa ushauri huo katika hafla ya  maadhimisho ya siku ya vyombo vya habari duniani kwa  mkoa wa kigoma  amesema serikali inatambua mchango wa waandishi wa habari katika kuchochea maendeleo ya mkoa wa kigoma  na taifa.

Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye, Picha na Tryphone Odace

Amesema ofisi ya mkuu wa mkoa itafuatilia viongozi wanaoficha taarifa na kushindwa kuzitoa kwa waandishi wa habari na kupelekea wananchi kushindwa kupata haki yao ya msingi ya taarifa.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa kigoma

Akizungumza katika maadhimisho hayo Rais wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo ametaja baadhi ya majukumu ya waandishi wa habari ikiwemo kutenda haki bila kumuumiza mtu, kuelimisha jamii na kuchochea uwajibikaji wa viongozi, huku baadhi ya viongozi klabu za waandishi wa habari kutoka nchini Burundi wakisema kuwa serikali imebadili baadhi ya sheria zinazowakandamiza waandishi wa habari.

Sauti ya viongozi wa vyama vya wanahabari

Nao baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa kigoma wamesema nikweli wapo baadhi ya viongozi  wa serikali ambao hawatoi ushirikiano kwa waandishi wa habari hivyo wananchi wanashindwa kupata taarifa za msingi zinazohusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Masuala mengine ambayo yamejadiliwa katika maadhimisho hayo ni waandishi wa habari kuandika taarifa kwa kufuata maadili, kuacha kuandika taarifa za uchochezi na kuimalisha umoja na mshikamano miongoni mwao na waandishi wengine kutoka nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya Burundi.