Joy FM

Wakimbizi waaswa kuacha uharifu kambini nyarugusu

10 May 2024, 15:16

Hawa ni wakimbizi na waomba hifadhi waliopo katika kambi ya nyarugusu Mkoani Kigoma Picha na Lucas Hoha

Serikali ya tanzania kwa kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa yamekemea vikali vitendo vya baadhi ya wakimbizi wanaojihusisha uhalifu ndani na nje ya kambi hiyo kwani imekuwa ikihatarisha amani kwa wenyeji wa tanzania.

Na Kadislaus Ezekiel – Kasulu

Wakimbizi na waomba hifadhi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanaohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya Kujihusisha na matukio ya uhalifu, ikiwemo mauwaji  ndani na nje ya Nchi kufuatia kuanza matukio hayo ndani ya kambi hiyo.

Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa Wakimbizi kutoka Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Sudi  Mwakibasi, Ametoa wito huo wakati akihutubia mamia ya Wakimbizi wa Nchi ya Kongo, ambapo amesema changamoto mbalimbali zinazowakabili zinashughulikiwa na jumuia ya Kimataifa na Serikali.

Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi Sudi Mwakibasi akizungumza na wakimbizi waliopo kambi ya nyarugusu, Picha na Lucas Hoha
Sauti ya Mkurugenzi idara ya wakimbizi Soud Mwakibasi

Katika Hatua Nyingine Kiongozi huyo, amesisitiza vijana kuacha kutumika katika machafuko, yanayopelekea hali ya usalama Nchini Kongo kuwa Ndogo.

Hatahivyo baadhi ya Wakimbizi wamesema suala la usalama kambini ni muhimu na watashirikiana na serikali kuhakikisha Wakimbizi wenye tabia za uhalifu wanachukuliwa hatua.

Wakimbizi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ndani ya kambi ya wakimbizi nyarugusu, Picha na Lucas Hoha

“Ni kweli wapo ambao wamepewa hifadhi hapa tanzania lakini unakuta wakitoroka na kufanya vitendo vya uharifu kwa wenyeji na jambo hili serikali na yele mashirika yashikamane kukomesha tabia hii kwani inasababisha tushindwe kusaidiwa wakati sisi ndo wenye matatizo ya kukimbia nchi yetu”