Joy FM

Madiwani watakiwa kusimamia miradi ya maendeleo

10 May 2024, 14:38

Mkuu wa wilaya kasulu kanali Isac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Miradi inakuwa kwenye maeneo yenu laikini hakuna hata anayejishughulisha kufuatilia kinachofanyika kwenye utekelezaji wa miradi na ndio maana tunakuwa miradi mingi ambayo haikidhi viwango.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amewaagiza madiwani wa kata zilizopo katika halmashauri ya wilaya Kasulu kusimamia vyema miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Kanal Mwakisu ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024

Amesema usimamizi wa baadhi ya miradi ya serikali hauakisi matumizi ya fedha ya mradi husika jambo linalopelekea kuisababishia harasa serikali kutokana na kushindwa kutekeleza kwa ubora unaotakiwa.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu

Aidha Kanal Mwakisu amesema miradi mingine inakuwa karibu na maeneo yao wanayoishi lakini wanashindwa kufuatilia hali inayosababisha wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo inakuwa na changamoto nyingi lakini endapo kama wangeisimamia ipasavyo isingekuwa na changamoto yoyote.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kasulu kanali Isac Mwakisu

Kwa upande wao baadhi ya madiwani wa kata katika halmashauri hiyo akiwemo diwani wa kata ya Bugaga Hitra Mlobelo na diwani wa kata ya Asante Nyerere Julius Mpwehuka wamesema uaminifu na kushirikishwa kwa kiongozi katika usimamia wa miradi ya maendeleo unatakiwa ili kuondoa kasoro kwenye miradi hiyo.

Sauti ya madiwani wa halmashauri ya wilaya kasulu