Ziwa Tanganyika kufungwa kwa miezi mitatu
10 May 2024, 12:38
Waziri wa mifugo na uvuvi Mh. Abdallah Ulega amesema shughuli za uvivi zitafungwa rasmi kuanzia may 15 hadi mwezi augost lengo ikiwa ni kulinda rasmali za ziwa tanganyika kuongeza.
Na Orida Sayon – Kigoma
Katika kutekeleza dhamira ya kulinda rasilimali za uvuvi ndani ya ziwa Tanganyika wadau na viongozi wa sekta ya uvuvi wametakiwa kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa mikopo kwa vijana na wanawake wanaojishughurisha na shughuli za uvuvi.
Wito huo umetolewa na Waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Abdallah Ulega katika mkutano wa kugawa vizimba na maboti ya kisasa ya uvuvi na doria kwa mikoa inayozunguka ziwa Tanganyika ikiwa ni Kigoma, Rukwa na Katavi.
Waziri Ulega pia ametoa tamko rasmi na elimu juu ya usitishwaji wa shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mei 15 ha agost 15 mwaka.
Mhe, Abdallah Ulega amesema Ongezeko la idadi ya wavuvi na vyombo vinavyotumika katika shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Tanganyika imepelekea upungufu mkubwa wa rasilimali zitokanazo na ziwa hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini mh, Shabani Kilumbe Ng`enda ametoa wito kwa wavuvi mkoani kigoma kuchukua vizimba ili pindi ziwa litakapofungwa waweze kuendelea kuvuna samaki ili kujikimu na mahitaji yao.
Baadhi ya wanufaika wa vizimba na maboti hayo kutoka mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi licha ya kuishukuru wameiomba serikali kusimamia na kudhibiti uvuvi haramu unaokabili shughuli za uvuvi ndani ya ziwa tanganiyika.