Udumavu pasua kichwa kigoma, mafisa lishe kikaangoni
9 May 2024, 12:58
Licha ya mkoa wa kigoma na wilaya zake kuzalisha aina mbalimbali za vyakula vya kutosha bado suala la lishe limekuwa gumu kwani bado watoto wanasumbuliwa na udumavu hali inayochangia hata watoto kushindwa kumudu masomo vizuri shuleni.
Na, Josephine Kiravu -Kigoma Dc
Katika kukabiliana na lishe duni kwa watoto wazazi/walezi katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma wametakiwa kuchangia chakula cha mchana shuleni kwa ajili ya watoto wao.
Hayo yamesemwa na Afisa lishe katika wilaya ya Kigoma Bw. James Swai wakati akiwasilisha taarifa ya lishe kwa kipindi cha mwezi January -March ambapo amesema mwitikio wa wazazi si mzuri huku akiainisha hali ya udumavu kwa mwaka jana ambayo ipo kwa asilimia 27%.
Kwa upande wake Afisa elimu Sekondari ambaye pia ni mratibu wa afya shuleni Flora Fundi amesema wanaendelea kuhamasisha wazazi juu ya kuchangia chakula kwa wanafunzi shuleni kupitia ziara na mikutano mbalimbali.
Hata hivyo kwa mujibu wa Afisa lishe wanaendelea kuhamasisha utoaji wa huduma ya chakula shuleni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za lishe shuleni