Meja Kodi: Lazima tulinde mipaka yetu iwe salama
7 May 2024, 17:00
“Mkoa wa Kigoma una wageni wengi wanaoingia nchini hivyo hatuna budi kuwa makini na kuhakikisha ulinzi unaimarika katika mipaka ya nchi yetu ili kuhakikisha hakuna tatizo linaokea”.
Na, Tryphone Odace – Kigoma
Mkuu wa Tawi la Lojistiki na Uhandisi Jeshini, Meja Jenerali Hawa Kodi amevitaka vikosi vya jeshi la kujenga taifa kuendelea kuhimiza ulinzi na uzalendo nchi kwa maaskari na vijana hasa kwa mikoa ilipo mpakani ikiwemo Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Lojistiki na Uhandisi Jeshini, Meja Jeneral Hawa Kodi amsema hayo mara baada ya kuzindua jengo la utawala na ofisi kuu ya kikosi cha jeshi la kujenga taifa 821 JK Bulombora ambapo amewata maaskari kuwa waadilifu na kuhakikisha wanasimamia viapo vya kuilinda mipaka ya nchi kutokana na kwamba baadhi ya mikoa ikiwemo kigoma ambayo imekuwa na mwingiliano wa raia kutoka nchi jirani.
Aidha amesema jeshi hilo litaendelea kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali kwa uwazi ambayo itasaidia kwenye ufinyu wa bajeti.
Awali Akitoa taarifa ya jingo hilo la utawala na ofisi kuu Kaimu Mkuu wa Kikosi cha 821 JK Bulombora Meja Msumi Seif amesema hadi kukamilika kwa jingo hilo limegharimu shilingi milioni 165 huku Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Juma Hongo akieleza kuwa jingo litakuwa msaada wa shughuli za maafisa wa jeshi hilo.