Joy FM

Mtoto wa miaka 8 afariki baada ya kuzama kwenye mto nyakafumbe

6 May 2024, 11:22

Ramani ikionyesha ramani ya wilaya za mkoa wa kigoma, picha na google

Wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili kubaini maeneo watoto wanapochezea ili kuwakinga kupata madhara na majanga ya kuanguka kwenye mito na visima.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Wananchi wa kitongoji cha Ruhuba kijiji cha Muhinda kata ya Muhinda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wanaendelea kuutafta mwili wa mtoto Elizaberth Alfred (8) mkazi wa kitongoji hicho mwanafunzi wa darasa la 1 shule ya msingi Ruhuba baada ya kuzama kwenye maji katika mto Nyakafumbe akiwa ameenda kuchota maji na watoto wenzake.

Zoezi la kuutafta mwili wa mtoto huyo leo ijumaa limeingia siku ya nne baada ya mtoto huyo kuzama kwenye maji siku ya jumanne aprili 30 akiwa ameenda kuchota maji na watoto wenzake.

Aksa Rashid na Alfred ntabagila ni wazazi wa mtoto huyo wamethibitisha kuwa tangu jitihada za kuutafta mwili zilipoaanza maara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa mtoto wao mpaka leo jitihada kumpata mtoto wao bado hazijafanikiwa.

Sauti ya wazazi wa mtoto wakieleza tukio

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha muhinda wilayani Buhigwe wamesema wazazi na walezi wanatakiwa kuwa walinzi kwa watoto wao ili kuwaepusha na majanga haya ambapo wamebainisha kuwa licha ya kusikitishwa na tukio hilo wametoa ombi kwa viongozi wa serikali kutoa msaada wa haraka yanapotokea matukio Yusta  ya dunia na Amos nyalema ni baadhi ya wananchi wa kijiji hicho.

Sauti ya wananchi wa kijiji cha Muhinda Buhigwe

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Muhinda bw. Jonas Damas alamba amesema mpaka sasa wanaendelea kushirikiana na familia kuutafta mwili wa mtoto huyo huku akieleza pia namna tukio lilivyotokea.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji ch Muhinda akieleza tukio la mtoto kuanguka kwenye kisima cha maji