Joy FM

Madaktari bingwa 60 kutoa huduma za kibingwa Kigoma

3 May 2024, 14:52

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa madaktari bingwa mkoani humo. Picha na Lucas Hoha.

Zaidi ya madaktari bingwa 60 wanatarajia kutoa huduma za afya za kibingwa kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma na mikoa jirani ikiwemo Tabora, Katavi pamoja na Rukwa kwa muda wa siku tano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni.

Mwandishi Lucas Hoha ana undani wa Taarifa hii.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya matibabu ya madaktari bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan kanda ya magharibi.

Andengenye ametaja baadhi ya huduma zitakazotolewa katika kambi hiyo ikiwemo matibabu ya mifupa, magonjwa moyo na magonjwa ya kinywa na meno.

Mkuu wa mkoa Kigoma: Thobias Andengenye

Aidha andengenye amesema kambi hiyo inalenga kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu ya kibingwa ambayo walikuwa wanalazimika kusafiri kwenda mikoa mingine, huku akiwaomba wananchi kujitokeza kupata matibabu hayo ili afya zao ziwe salama.

Mkuu wa mkoa Kigoma: Thobias Andengenye

Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dkt. Stanley Binagi ameshukuru serikali kwa juhudi wanazozifanya za kuendelea kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi wa mkoa wa kigoma kwani hali ya sasa imeboreshwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Mganga Mfawidhi: Dkt. Stanley Binagi