Wahudumu wa afya acheni lugha chafu kwa wagonjwa
3 May 2024, 12:06
Mkuu wa wilaya Kigoma Mkoani kigoma amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali wahudumu wa afya wanaokiuka madili ya kazi zao kwa kutumia lugha chafu kwa wagonjwa ikiwmo kuwasimamisha kazi.
Na Orida Sayon – Kigoma
Wahudumu wa vituo vya Afya na zahanati katika Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma wametakiwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu badala ya kutumia lugha zisizo za staha kwa wagonjwa.
Hapa ni katika kituo cha Afya cha Buhunda kilichopo kata ya Buhunda katika manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo imefanyika hafla fupi ya uzinduzi wa jengo la wodi ya wazazi na kukubidhi Gari la kubeba wangonjwa na hapa Mkuu wa wilaya ya kigoma Mh. Salum Kali anawataka watumishi kuwa lugha nzuri kwa wagogonjwa.
Amesema kumekuwa na wahudumu ambao wamekuwa hafuati kanuni na miiko ya kazi yao na hivyo kushindwa kufanya kazi ya uuguzi na kutoa huduma kwa wagonjwa jambo ambalo linasababisha wananchi waendelee kuona hawapati huduma bora zaafya wakati serikali ikiwa inaendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya.
Uzinduzi huo umefungua njia ya upatikanaji wa huduma nyingine ikiwemo mashine ya ultrasound kwa vituo vya afya vitatu Gungu, Buhanda na ujiji pamoja na huduma ya Damu salama kama anavyoeleza Mganga mkuu Manispaa ya kigoma ujiji Bw.Hashimu Mvogogo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buhanda Bw.Kilahumba Gilbert Lutuli ameitaka serikali kukamilisha miundombinu ambayo bado haijakamilika.
Na baadhi ya wananchi kutoka katika kata hiyo wameeleza hisia zao mara baada ya kupata jengo la wazazi kituoni hapo.