Joy FM

Dc kasulu akerwa na vitendo vya uvunjifu wa amani

1 May 2024, 13:29

Mkuu wa Wilaya Kasulu akiungumzia hali ya ulinzi na usalama wilaya kasulu, Picha na Michael Mpunije

Vitendo vya wizi na uharifu kwenye jamii wilayani kasulu vimeendelea kuumiza vichwa kwa viongozi huku wananchi wakiendelea kuumia kwa mali zao kuibiwa na wengine kuharisha maisha yao.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wananchi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kutoa taarifa za viashiria  vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza katika jamii ili kudumisha amani na kujiletea maendeleo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaack mwakisu wakati akizungumza ofisini kwake kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.

Kanali Mwakisu amesema jukumu la ulinzi ni lakila mmoja hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha amani inatawala jambo ambalo litasaidia wananchi kufanya shughuli za uzalishaji kwa uhuru.

Sauti ya Mkuu wa wilaya kasulu

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakazi wa mtaa wa boma kata ya Kimobwa halmashauri ya mji Kasulu wamesema wanashirikiana na viongozi wa serikali katika kutoa taarifa za matukio ya uhalifu huku wakisisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wananchi.

Sauti ya wananchi wilayani kasulu

Hata hivyo nimezungumza kwa njia ya simu na Mkuu wa kitengo cha polisi jamii kutoka makao makuu ya polisi Dodoma kamishina msaidizi wa polisi ACP Elisante Ulomi kuhusu umuhimu wa wakushirikiana na wananchi kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu.

Sauti ya mkuu wa kitengo cha polisi makao makuu Dodoma