Shilingi bilioni 2.7 kutekeleza miradi ya afya na elimu kibondo
1 May 2024, 13:06
Serikali imesema itaendelea kusimamia na kutoa kipaumbele kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuwafikishia huduma wananchi.
Na James Jovin – Kibondo
Halimashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kupitia ruzuku ya serikali kuu imepokea fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali hususani katika eneo la utawala, elimu na afya.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya Mipango katika halimashauri ya wilaya ya Kibondo bwana Daud Mapunda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa irani na miradi inayotekelezwa.
Aidha amesema kuwa fedha hizo zinaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala, vyumba vya madarasa, kituo cha afya kimoja na zahanati mbili katika vijiji vya Kasana na Nyaruranga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kibondo bw. Hamisi Tahilo amepongeza halimashauli ya wilaya ya Kibondo kwa kutekeleza miradi kwa viwango vinavyotakiwa na hii ni baada ya kamati ya siasa kutembelea miradi hiyo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Deocles Rutema richa ya pongezi hizo amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa