Wavuvi mialoni wageuka mwiba kwa wanawake
1 May 2024, 10:31
Vitendo vya ukatilii hasa kubakwa maeneo ya mialo mbalimbali mwambao wa ziwa tanganyika vimeendelea kuacha kovuna simanzi kwa wananwake wanaojishughulisha na uchakataji wa mazao ya samaki.
Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma
Wanawake Wanaochakata Mazao ya Uvuvi Katika Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma, wamelalamikia wenza wao wa ndoa hasa Wavuvi, kutelekeza Familia zao, na kuwatuhumu kushinda kwenye vijewe vya kahawa bila kufanya kazi, na baadhi yao wakiacha Familia Kwa kuwatelekeza katika mialo Mingine ya Uvuvi, na Watoto kukosa malezi ya Baba.
Wamesema hayo wakati wa mkutano wa wadau wa uvuvi na viongozi, katika Mwalo wa Katonga Mjini Kigoma, uliondaliwa na Shirika la FAO chini ya Mradi wa FISH4ACP, Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine SUA kampasi ya Mizengopinda Katavi, kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika mnyololo mzima wa Uvuvi.
Katika kikao hicho cha wadau wa Mazao ya Uvuvi, Zaituni Hassan na Zubeda Fadhili, wamesema wavuvi wanatelekeza familia zao, kwa kuhama katika mialo mingine kulingana na kufuatauvuvi kwa misimu huku familia zikisalia na malezi ya Mama tuu na kukosa msaada kutoka kwa Mzazi wa Kiume.
Hatahivyo, Mmoja wa wanawake ambaye ni mchakataji wa mazao ya Uvivi ziwa Tanganyika katika mwalo wa Katonga, Bi Chausiku Issa amewapongeza wanaume wanaojali familia zao na kuhakikisha malezi kwa watoto yanazingatiwa, kwa kuwa wanatengeneza kizazi bora chenye malezi kamili kutokakwa Baba na Mama.
“Wanaume wanaojali familia zao, wanapaswa kupongezwa kwa kuwa wanajenga kizazi bora, chenye malezi bora, amani na upendo kwa wazazi na watoto, na jamii inatakiwa kuhakikisha inathamini na kujali malezi’
Mtafiti na mshauri wa masuala ya maendeleo kutoka chuo kikuu cha Sokoine SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi, Profesa Anna Sikira pamoja na Afisa Uvuvi Manispaa ya Kigoma Ujiji Edmond Scauti wamewataka wanaume kutunza familia zao, licha ya kuwa Wanahama mara kwa mara kwa shughuli za uvuvi.