Vijana wa JKT Bulombora lindeni amani, acheni dawa za kulevya
1 May 2024, 10:07
Vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi Katika kambi ya jeshi la kujenga taifa 821 KJ Bulombora iliyopo wilayani Kigoma Mkoani Kigoma wametakiwa kuwa wazalendo Katika kuilinda Nchi kama sehemu ya kiapo walichopewa wakati wa mafunzo hayo.
Na Tryphone Odace – Kigoma
Katika Taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, iliyosomwa na Mkuu wa Tawi la Utawala Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesisitiza vijana wanaohitimu mafunzo ya kijeshi kuwa wazalendo katika kudhibiti uhalifu na wahalifu.
Naye Kamanda wa kikosi 821 KJ Bulombora Luteni Kanal Juma Hongo, amesema hadi vijana hao wanahitimu wanafanikiwa kufuzu mafunzo mbalimbali ya kijeshi na vijana wakieleza kujiepusha na matumizi ya Dawa za Kulevya.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salumu Kalli akifunga mafunzo hayo ya vijana Oparesheni Miaka sitini ya Jeshi la Kujenga Taifa, Katika Kikosi 821 KJ Bulombora amewasisitiza kuwa wadilifu kwa jamii na taifa kwa ujumla.