“Nchi yetu imeanza kuchukua hatua,matumizi ya gesi”
26 April 2024, 09:39
Matumizi ya nishati ya kupikia itasaidia kutunza mazingira yetu kwani kwa sasa mafuriko tunayoyaona ni matokeo ya uharibifu wa mazinira na misitu kwa kukata miti na misitu.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kutumia nishati safi ya kupikia na kuepuka matumizi ya kuni yanayopelekea uchafuzi wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanal Isaac Mwakisu wakati wa tamasha la usiku wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambayo yamefanyika aprili 25 katika uwanja wa umoja uliopo mjini Kasulu
Kanal Mwakisu amesema katika maadhimisho ya sherehe za Muungano ni vyema wanachi kuona umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia ili kufikia maendeleo endelevu katika ujenzi wa taifa.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako amesema ushirikiano wa wananchi na viongozi umpelekea Muungano kuimarika zaidi.
Nao baadhi ya wananchi wilayani Kasulu akiwemo Elisha Kebero na Bathoromeo Malaki wamesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeongeza fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa Tanzania.
Kaulimbiu ya miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania âTumeshikamana na tumeimarika kwa maendeleo ya taifa letu.