Wanachuo Kasulu wakosa vifaa vya kujifunzia
25 April 2024, 14:49
Serikali imeombwa kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kujifunzia wanafunzi wa chuo cha ualimu kaslu Mkoani Kigoma.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Chuo cha Ualimu Kasulu (Kasulu TTC) kilichopo halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma kinakabiliwa na changamoto ya vifaa vya kufundishia hali inayopelekea wanachuo kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao yakiwemo masomo ya sayansi
Ni katika awamu ya 38 mahafari ya 39 ya chuo cha ualimu Kasulu ambapo katika risala iliyosomwa na rais mstaafu wa serikali ya wanachuo Bw. Zabron Njamajame amesema mbali na mafanikio ambayo wameyatapa amezitaja pia baadhi ya changamoto hizo kuwa zinakwamisha ufaulu kwa wananchuo.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha ualimu Kasulu Zawadi Ngereja amesema wanachuo hao wameandaliwa vizuri na wamejengewa uwezo wa kutoa elimu kwa jamii ili kuwaandaa vijana wenye uwezo wa kuliongoza taifa.
Naye mgeni rasmi katika mahafari hayo Meneja wa NMB wilaya ya Kasulu ndugu. Ipyana Mwakatobe amesema atazifanyia kazi changamoto zote zinazowakabili wanachuo hao.
Jumla ya wananchuo wa kada mbali mbali ambao wamehitimu ni 266 kutoka ngazi tofauti ambapo wanawake ni 125 na wanaume ni 141