Dc kasulu awakalia kooni wahudumu wa afya
23 April 2024, 13:23
Wahudumu wa afya ngazi Wilayani kasulu wametakiwa kuzingatia maadili na taratibu za utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Na Michael Mpunije – Kasulu
Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu amekemea lugha zisizo za staha zinazotolewa na baadhi ya wahudumu wa afya wa zahanati, vituo vya afya na hospitali wilayani humo kuwa zinaleta taswira mbaya kwa wagonjwa na kuwakatisha tamaa
Katika kikao kazi kilichowakutanisha watoa huduma za afya wa zahanati,vituo vya afya na hospitali katika halmashauri za kasulu mji na kasulu vijini kimelenga kuhamasisha huduma bora za afya pamoja na kushirikiana kutatua baadhi ya changamoto katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Isaac mwakisu amesema wahudumu wa afya ambao watabainika kutoa lugha zisizo za staha kwa wagonjwa watachukuliwa hatua za kisheria badala yake wanatakiwa kutoa huduma bora za afya.
Kwa upande wake katibu Tawala wilaya ya Kasulu Bi,Theresia mtewele amesema watoa huduma za afya wanatakiwa kuwa waaminifu kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na kuepuka wizi wa baadhi ya dawa na vifaa.
Jumla ya maadhimio 15 yamefikiwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wahudumu wa afya kuhakikisha wanatunza siri za wagonjwa kama anavyoeleza katibu tawala heru juu bw. Sabato Kizeba.