Dc kigoma msiogope chanjo kama mlivyokimbia chanjo ya corona
22 April 2024, 14:12
Takwimu za Shirika la umoja wa mataifa la Tafiti za Saratani za mwaka 2020, zinaonesha kuwa tatizo la saratani ya matiti na mlango wa kizazi nchini Tanzania limekuwa likiongezeka mara kwa mara, ambapo katika watu 100,000 watu 10 hugundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi
Na Josephine Kiravu – Kigoma
Zaidi ya watoto wakike laki 2 na elf 31 wenye umri wa kati ya miaka 10 -14 wanatarajia kufikiwa na kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kigoma.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa utoaji chanjo hiyo kwa Mkoa wa Kigoma, Mganga Mkuu Mkoa wa huu Dr Jesca Leba amesema mpaka sasa wamepokea chanjo zaidi ya laki 2 na elf 80 kwa ajili ya kuwachanja wasichana walio katika umri huo ili kuwalinda na athari zitokanazo na saratani ya mlango wa kizazi.
Naye Kaimu Mratibu wa chanjo Mkoa wa Kigoma Deltus Sevelin amesema wanaendelea kuelemisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hii ambayo itatolewa kwenye maeneo ya shule na vituo vya afya na kwamba lengo ni kufikia angalau asilimia 80%.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya kigoma akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewataka wazazi na walezi kuachana na mitazamo hasi kuhusu chanjo na kwamba chanjo hii ni salama.
Nao baadhi ya watoto wakike ambao wamepatiwa chanjo wameeleza mitazamo yao kuhusu chanjo hiyo huku wakiwataka wazazi kutowanyima watoto wao kupata chanjo hiyo kwani ni salama.