Suluhisho kupata viongozi bora Kigoma lapatikana
22 April 2024, 12:56
Wazazi na Walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema ambayo yatawasaidia kuwa viongozi bora katika jamii inayowazunguka.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa kanda ya kati wa kanisa la Anglikana Nyumbigwa Dayosisi ya Western Tanganyika Mchungaji Canon Aron Kimuzanye wakati akizungumza na radio joy fm ndani ya ofisi za kanisa la anglikana parish ya Nyansha lililopo halmashauri ya Mji Kasulu
Amesema taifa au taasisi yoyote ya kidini haiwezi kuwa na viongozi waadilifu endapo kama wazazi au walezi hawata husika kuwapatia malezi bora watoto wao.
Kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglikana Nyansha Eliud Katore amesema mzazi au mlezi anaposhindwa kumlea mtoto wake katika maadili mema itasababisha kufanya vitendo viovu ambavyo havifai katika jamii.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wa kutoka wilayani Kasulu akiwemo Neema Chuma, Jackson Msore na Sephania Mbogamo wamesema mtoto anajifunza tabia njema kutoka kwa mzazi wake hivyo mzazi anatakiwa kuishi vizuri na mtoto wake ili aweze kukua katika maadili yatakayompendeza Mungu na jamii kwa ujumla
Maandiko matakatifu yanasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee