Udamavu kwa watoto kigoma pasua kichwa
22 April 2024, 09:02
Viongozi Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia huduma za afya na lishe kwa usahihi ili kunusuru watoto kuandamwa na tatizo la udumavu licha kuwa ni mkoa unazalisha vyakula vya kutosha
Na Kadislaus Ezekeil – Kigoma
Nchi za Tanzania na Marekani zimezindua mradi wa miaka mitano wa lishe unaolenga kupunguza udumavu kwa watoto waliochini ya miaka mitano, katika mikoa mitano ya Tanzania bara ambayo hali ya udumavu inaonekana kuwa juu na kuathili watoto wengi.
Mradi huo unatekelezwa chini ya shirika la maendeleo la serikali ya marekani USAID na wadau wengine, kwa thamani ya dora za marekani milioni 40, matarajio ikiwa ni kuwa na jamii yenye afya bora.
Viongozi mbalimbali akiwemo katibu tawala mkoa wa Kigoma Hassan Abbas pamoja na mkurugenzi wa mipango na bajeti ofisi ya Waziri mkuu, sera, Bunge na uratibu Eleuter Kihwele, wamesema serikali imekuwa ikipambana kwa ukamilifu Dhidi udumavu, na kwamba mradi huo utachochea mapambano dhidi ya udumavu.