Halmashauri ya Kibondo kujenga jengo la ghorofa 3
7 February 2024, 14:32
Halmashauri ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imetenga shilingi bilioni 2.5 ili kujenga jengo jipya la vijana community center ikiwa ni mikakati ya kuchochea na kukuza uchumi wa halmashauri na jamii kwa ujumla
Na, James Jovin
Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Kibondo mjini Bw. Alex Baragomwa wakati akizungumza na radio Joy na kwamba jengo hilo la gholofa tatu litakuwa na vibanda vya biashara, ofisi, ukumbi wa mikutano na maegesho ya magari.
Aidha ameongeza kuwa ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2024/2025 hivyo litakapokamilika litasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla
Katika hatua nyingine amesema kuwa kupitia mapato ya Ndani halmashauri imetenga bajeti ya shilingi milioni 292 kwa ajili ya kujenga vibanda vya biashara katika mji wa kibondo sambamba na ujenzi wa soko la samaki soko ambalo lilikuwa kikwazo kwa wananchi hasa matope wakati wa mvua.