Mkuu wa wilaya Kasulu ainyoshea kidole Tanesco
18 January 2024, 17:03
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanal Isaac Mwakisu amemtaka meneja wa tanesco kuhakikisha wilaya inakuwa na umeme wa uhakika kutokana na ongezeko la viwanda vidogo vodogo ambavyo haviwezi kuendesha shughuli zake bila nishati hiyo.
Kanal Mwakisu amesema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya kasulu ambapo amesema kama kata kata ya umeme ya mara kwa mara ikiendelea itasababisha maendeleo ya wilaya kurudi nyuma kutokana na kupungua kwa uzalishaji.
Amesema iwekwe miundombinu imara ya umeme ambayo itasaidia kupunguza kero ya kuwepo kwa umeme ambao unakuwa hauna nguvu na kwamba hii itasaidia kuendelea kuwekeza wilayani humo.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco wilaya ya Kasulu Danford Yungu amesema kukamilika kwa mradi wa umeme wa grid ya taifa utatatua changamoto ya huduma hiyo wilayani Kasulu