Afariki baada ya kufukiwa na kifusi cha mawe Kigoma
6 October 2023, 16:21
Jamii imeomba Serikali kuchukua hatua za kudhibiti shughuli za uchimbaji wa madini ya mawe katika eneo la masanga manispaa ya kigoma Ujiji kutokana na kuhatarisha maisha ya watu.
Na Eliud Theogenes
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Shabani amefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati akichimba mawe katika mgodi wa mawe uliopo katika Mtaa wa Masanga Kata ya Gungu Manispaaa ya Kigoma Ujiji.
Akizungumza na Kituo hiki Ndugu wa marehemu Bw. Adam Mikidadi, anaeleza namna mauti ilivyomfika Shabani huku baadhi ya wananchi wakiomba hatua zichukuliwa ili usalama uwepo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mgodi huo anaelezea kiundani namna tukio lilivyotokea.
Mwenyekiti wa mtaa wa Masanga kata ya Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji anathibitisha namna Ajali ilivyotokea na anaiomba serikali kuingilia kati suala hilo na kuwa hilo ni tukio la pili ndani ya mwezi mmoja.
Hata hivyo Jeshi la polisi limefanikiwa eneo la kuondoka mwili wa marehemu kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine za kiuchunguzi.