Halmashauri ya Kasulu mji yafikia lengo la utoaji wa chanjo ya polio
27 September 2023, 12:20
Halmashauri ya mji Kasulu mkoani kigoma imefanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 128 katika utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 iliyoendeshwa kwa muda wa siku nne.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Chanjo halmashauri hiyo Itumbi Munisi wakati akizungumza na Radio Joy fm katika kituo cha afya Kiganamo ambapo amesema wamevuka lengo walilokuwa wamejiwekea la kutoa chanjo ya polio kwa watoto 86,760.
Aidha Munisi amewaomba wazazi na walezi kuwa na mwamko wa kuitikia chanjo kwa ajili ya watoto wao kwani mtoto anaposhindwa kupata chanjo hii itasababisha kupata ulemavu au kifo.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema ni vyema kila mzazi akaona umuhimu wa kumpeleka mtoto wake kupatiwachanzo ya polio ya matone kwani haina madhara yoyote kulingana na walivyo elekezwa na wataalamu wa afya
Utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 ulianza mnamo septemba 21 -24. 2023 na wameongeza siku nyingine mbili ili kuhakikisha wale ambao hawakuwa wamefikiwa kupata chanjo hiyo wanafanikiwa.