Sekta binafsi zatakiwa kutenga fedha kwa ajili miradi ya maendeleo
4 August 2023, 17:04
Mashirika yasiyo ya kserikali yametakiwa kuhakikisha wanatumia fedha za wafadhili katika kutekeleza miradi ya maendeleokwenye maeneoyao.
Na Lucas Hoha
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina Mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amezitaka Sekta binafisi kutenga fedha kwa ajili ya kutekeza miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa jamii katika Sekta muhimu ya miundombinu ya Elimu, Barabara na Maji
Andengenye ametoa wito huo Kwenye kilele cha Mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuna kila sababu ya mashirika hayo kuelekeza nguvu kwenye sekta hizo pamoja na kujenga uwezo wa kujiendesha badala ya kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili.
Kwa Upande wake Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Albert Msovela Amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yako 196 ndani ya Mkoa huo, huku akiongeza kuwa licha ya mafanikio ambayo Mkoa wa Kigoma umeyapata kupitia mashirika hayo yale mashirika ambayo hayako hai Ofisi itayafutia usajili.
Naye Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Kilumbe shabani Nge’nda amesema Sekta binafisi ni nguzo ya maendeleo ya Taifa, huku Mjumbe wa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali Kutoka KONGO, Angelo Tungaraza akisema kuwa wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo
Masuala mengine ambayo yamejadiliwa katika Mkutano huo ni kuyataka mashirika yasiyo ya Serikali kushirika kikamilifu katika kukemea vitendo viovu ndani ya jamii, kupinga na kupiga vita ukatili wa kijinsia, na kutoa Elimu kwa jamii ya watanzania kuyaishi maadili ya nchi yao