Jamii yatakiwa kuzingatia maadili
4 August 2023, 10:09
Maadili nchini yanaonekana kuendelea kuporomoka hali inayosababisha jamii kuendelea kupotoka na kusababisha jamii kuwa katika hali ngumu ya maisha hasa kufanyiwa ukatilii.
Na, Josephine Kiravu
Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa Kujiepusha vitendo vilivyo kinyume na maadili ya Kitanzania kuanzia ngazi ya familia,Taasis za Umma na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kulinda kizazi Kijacho katika Nyanja mbalimbali Nchini
Rai hiyo imetolewa na Katibu msaidizi Kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili na Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Gerad Mwaitebele akiwa katika mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma
Mwaitebele Amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayo nafasi katika kuelimisha jamii kuendeleza na kudumisha Uzalendo, Maadili na Kuchukia maovu ikiwa ni pamoja na kumsaidia mwananchi kufikisha malalamiko yao .
Kwa upande wao baadhi ya wadau kutoka Taasis mbalimbali zisizo za kiserikali akiwemo, wamesema Utandawazi na wasanii wa sanaa hasa ya muziki na maigizo wamechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu maadili kwenye jamii nchini.
Mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kigoma ambao umeanza hspo Jana unatarajia kufikia tamati hapo kesho huku suala la maadili na uwazi likiendelea kusisigizwa na viongozi mbalimbali akiwemo Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Kigoma.