Wakimbizi waishio kambi ya Nyarugusu wagoma kurudi kwao Burundi
2 August 2023, 01:11
Serikali nchini Tanzania imesema itaendelea kuhamasisha wakimbizi waliopo katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu kurudi nchini Burundi kutokana na amani iliyopo kwa sasa.
Wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma nchini Tanzania wameiomba serikali ya Burundi kutatua matatizo ya kifamilia na usalama ili waweze kushawishika kurudi nchini kwao.
Na, Tryphone Odace
Baadhi ya wakimbizi hao akiwemo Frederick Ntankiza Imana na Ndaishimiye Diodone wamesema hayo baada ya ujumbe kutoka Burundi wa kuhamasisha wakimbizi kurudi kwao na kuwa wana hofu kutokana na ukosefu wa usalama na makazi ya kufikia kutokana wengi wao kukaa kambini muda mrefu.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya ndani nchini Tanzania Sudi Mwakibete amesema wakimbizi hao ni bora wakarudi ili wakaijenge nchi yao na kuwa mpaka sasa takribani wakimbizi 4,000 wamejiandisha kurejea kwao.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Burundi Kalemiye Mbarushimana amesema wanaendelea kuwashawishi wananchi wao ili waweze kurudi nyumbani kwani tayari serikali imekwishaweka mazingira ya kuwapokea na wataishi salama.
Kambi ya wakimbizi Nyarugusu ilianzishwa mwaka 1996 na ina jumla ya wakimbizi laki moja elfu thelathini na saba na mia tisa themanini na tisa ambao walikimbia machafuko nchini Burundi na Congo.
Kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu walijiandikisha na kurejea nchini kwao.