Joy FM

Madiwani Kasulu mji wachagua makamu mwenyekiti

2 October 2024, 09:10

Madiwani halamashauri ya mji kasulu wakiwa katika zoezi la kumchagua Diwani seleman kwirusha kuwa makamu mwenyekiti wa halamshauri, Picha na Emmanuel Kamangu

Madiwani katika halmshauri ya mji wa Kasulu Mkoani kigoma wamesema kuwa wataendelea kumuunga mkono makamu mwenyekiti aliyechaguliwa kwa mara ya nne ili kuahkikisha wanatekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo ndani ya wilaya hiyo.

Na Emmanuel Kamangu – Kasulu

Baraza la Madiwani halamashauri ya mji kasulu mkoani kigoma wamemchagua Diwani seleman kwirusha kwa mara ya nne kuwa makamu mwenyekiti wa halamshauri hiyo.

Makamu mwenyekiti  ambaye amechaguliwa kwa awamu ya nne Bw, kwirusha amewashukuru kwa dhati waheshimiwa madiwani kwa kumuamini huku akiwaomba ushirikiano  madiwani wote  ili kusukuma gurudumu la maendeleo kikamilifu.

Pichani ni Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Mji wa Kasulu Seleman Kwirusha ambaye amechaguliwa, Picha na Emmanuel Kamangu
Sauti ya Makamu mwenyekiti  ambaye amechaguliwa kwa awamu ya nne Bw. kwirusha

Diwani  wa kata ya nyasha Bw, Patrick Madaraka ni mmoja wa madiwani ambao wamempongeza Bw, Kwirusha kwa kushinda  kiti hicho  huku akiwasirihi madiwani  wenzake wa  ccm kushikamana na kuacha misuguano inayoweza kuchelewesha shuguli za maendeleo.

Sauti ya Diwani  wa kata ya nyasha wilayani kasulu Bw. Patrick Madaraka

Aidha miongoni mwa viongozi ambao wamechaguliwa kwenye  kamati tatu za kudumu za halmashauri  ni pamoja na kamati ya uchumi , elimu na afya Diwani Emmanuel Gamuye, sambamba na kamati ya mpango mji ,ujenzi na mazingira diwani Ezron Budurege.