Joy FM
Joy FM
13 March 2026, 14:36

Watumishi wa afya 6 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamefariki baada ya kupinduka kwa boti waliyokuwa wakiitumia kwenda kusambaza dawa katika katika eneo la Kagunga Wilaya ya Kigoma.
Jumla ya watu sita wamefariki na wengine 9 wameokolewa kufuatia ajari ya boti iliyokuwa imebeba watu 18 kutokea Kigoma Mjini kwenda Kagunga ndani ya Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Kalalangabo Wilaya ya Kigoma.
Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema boti hiyo ilikuwa imebeba watumishi wa serikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambao wote wako Idara ya Afya, huku akitoa ushauri kwa wananchi kufuata utabiri wa watu wa hali ya hewa kalba ya kusafiri Ziwani.
Michael Maganga ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma amesema chanzo cha ajari hiyo ni wimbi kubwa la maji lililotokea ndani ya Ziwa Tanganyika muda mfupi baada ya watumishi hao kuanza safari.

Kwa upande wao, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema wamesikitishwa na ajali hiyo kwani ndiyo mara ya kwanza kutokea eneo lao.
Kati ya hao watu hao waliofariki miili sita imeokolewa huku mingine mitatu juhudi zikiwa zinaendelea za kuitafuta.