Joy FM

Watoto yatima wapewa msaada na kanisa la Anglikani Kigoma

13 February 2026, 10:05

Watoto wanaolelewa kituo cha Matyazo wakiwa kwenye picha na waumini wa kanisa la Anglikani wkiwa wametoa misaada kwa watoto hao, Picha na Prisca Kizeba

Watoto yatima ni sehemu muhimu ya jamii yetu na hawa ni watoto waliopoteza wazazi wao au walezi wao, hivyo hukosa malezi, ulinzi na msaada wa karibu wa kifamilia na kutokana na hali hiyo, watoto yatima hukumbana na changamoto nyingi kama ukosefu wa mahitaji ya msingi, elimu, na msaada wa kihisia.

Na Prisca Kizeba

Jamii Mkoani Kigoma imeaswa kuwasaidia watoto  waliopo katika manzigira hatarishi hasa watoto yatima wanaoishi katika vituo vya kulea watoto.

Hayo yamesemwa na Mgurungenzi wa Kanda ya Manispaa ya Kigoma Mchungaji  Kanoni Andasoni Bilasa wakati akigawa zawadi kwa watoto yatima katika kituo cha Matyazo kilichopo Kata ya Kalinzi Halmashauri ya Wilaya Kigoma na kuwa jamii inatakiwa kuwa na upendo na huruma katika kuwahudumia watoto yatima

Mchungaji Kanoni amezitaja zawadi hizo kuwa  zimegharima  shilingi milioni tatu laki tatu na mia tano na wameguswa kama kanisa la Anglikana Kanda ya Manisapaa kwa kuwatembelea watoto hao.

Watoto wanaolelewa kituo cha Matyazo wakiwa kwenye picha na waumini wa kanisa la Anglikani wkiwa wametoa misaada kwa watoto hao, Picha na Prisca Kizeba

Akipokea zawadi hizo, Mwangalizi na mlezi wa watoto hao Bi. Ziada  Yasin ameshukuru kanisa la Anglikani Kanda ya Manisapa na kuwa zawadi walizotoa zimegusa moja kwa moja mahitaji ya watoto na kuomba tasisi zingine kuendelea kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Nao baadhi  ya viongozi wa kanisa hilo akiwemo mwenyekiti wa msafara huo Fanuel Magambo na Mama Mkurugennzi wa kanda hiyo Dorcas Bilasa  wameeleza namna gani wamekuwa na msukumo wa kuwatembelea watoto hao.